Jukwaa huru la Steemit, Mtandao Wa Kijamii wenye kulipa

in jukwaa •  8 years ago 

Jamani tuchangamkie fursa hii ya kipekee kuwajulisha wenzetu juu ya hili jukwaa la Steemit. Wengi hawafahamu kuwa katika Steemit unaweza tengeneza hela kwa kuwakilisha makala mbali mbali na pia kuunga mkono makala za wengine. Ukiwa na wafuasi wengi basi unakuwa na uwezekano mkubwa sana wa kutengeneza kipato cha Steem ambacho unaeza badilisha kwenda bitcoin na kisha kwenye pesa zako za makarasi.

Nawapenda wana familia wa steemit. Tukichangamkia hii fursa na kuitumia vizuri, nina imani wengi wetu tutanufaika vizuri sana
Wengi tumekuwa tukitumia Facebook kuposti picha zetu mbalimbali lakini imekuwa hatulipwi chochote. Lakini katika jikwaa la steemit ni tofauti, hapa unaeza lipwa fedha za kidigitali za steem ambazo baadaye waweza zibadili kwenda katika dola za kimarekani au za nchi yako..

Mimi nashukuru sana kwa kupitia Ethtrade nimeweza kuijua Steemit ambayo naamini itaniletea manufaa makubwa ikiwa nitaitumia vyema.

Naomba anayefahamu Kiswahili basi tutumie jukwaa hili kikamilifu.

Mimi nipo Dar es salaam. napenda yeyote mwenye mawazo ya kuchangia basi anifuatilie ili tuweze kushirikiana katika elimu hii.

Asanteni na Karibuni!

Geofrey a.k.a Litemi

Authors get paid when people like you upvote their post.
If you enjoyed what you read here, create your account today and start earning FREE STEEM!